PROF. TIBAIJUKA AWATOLEA UVIVU WALIOVAMIA MAENEO YA WAZI SINZA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PROF. TIBAIJUKA AWATOLEA UVIVU WALIOVAMIA MAENEO YA WAZI SINZA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali.
Diwani wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E wengine ni waandishi wa habari walioongozana na Waziri Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages