VODACOM MISS TANZANIA SALHA ISRAEL AKABIDHI FULANA 1000 KWA MKOA WA RUKWA NA KATAVI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM MISS TANZANIA SALHA ISRAEL AKABIDHI FULANA 1000 KWA MKOA WA RUKWA NA KATAVI

Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akifurahia jambo wakati akimkabidhi fulana Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom imekabidhi fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kushoto na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Salum Mwalim wakijadili jambo na Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel wakati wa makabidhiano ya fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne zilizotolewa na Vodacom Tanzania,kwa ajili ya kufanikisha tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho jijini Dares salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole kulia akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho mara baada ya Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel(katikati) kumkabidhi msaada wa fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne zilizotolewa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages