MKUU NIMEFURAHISHWA NA LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU" - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUU NIMEFURAHISHWA NA LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU"

https://mail.google.com/mail/?ui=2&ik=3530edf2ab&view=att&th=133de31891447062&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_gvg4svs70&zw 
Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages