Mama
Salma Kikwete(kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama
Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa ya mdogo wake na Rais
Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete mjini Bagamoyo Hivi Karibuni.
--
MKE
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia
Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa kundi jipya
la Taarab na albam ya kwanza ya kundi hilo, ambalo kwa sasa limekuwa
gumzo kubwa kwa mashabiki wa muziki wa Taarab Nchini, Tanzania Modern
Taarab (T-Moto) ama Real Madrid.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini,
alisema kuwa uzinduzi wa kundi hilo ulisogezwa mbele hadi kesho Ijumaa,
badala ya tarehe ya kwanza iliyokuwa imepangwa ya oktoba 28, kutokana na
ukumbi huo kuwa na shughuli ya ghafla ya Waziri Mkuu katika tarehe hiyo
iliyokuwa imepangwa kufanyika uzinduzi huo.
Aidha Amini alisema kuwa baada ya ratiba hizo kuingiliana katika ukumbi huo mmoja wa Diamond Jubilee, ilibidi
kundi hilo kusitisha na kusogeza mbele uzinduzi wake ambapo kwa sasa
maandalizi yote kuhusu uzinduzi tayari yamekamilika.
Amini
alivitaja vikundi vitakavyosindikiza onyesho la uzinduzi huo kuwa ni
pamoja na Bendi mahiri inayoundwa na vijana watatu, Mapacha wa3, Bendi
kongwe nchini, Msondo Ngoma, Sabaha Salum, anayeimba miondoko ya Taarab
pamoja na Kikundi cha Sanaa cha Twins Voice, kinachoimba nyimbo za
kuhamasisha kujilinda dhidi ya magonjwa ya Ukimwi.
Pia
Amini alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa mashabiki wote wataingi
ukumbini kushuhudia onyesho hilo kwa kulipa sh, 10,000 tu, ambapo pia
baada ya uzinduzi huo zitapatikana Kanda za albam hiyo zitakazokuwa
zikiuzwa ukumbini humo.
Mwisho.....
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)