MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA ENEO LA SOKO LA MWANJELWA JIJINI MBEYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA ENEO LA SOKO LA MWANJELWA JIJINI MBEYA

  Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa mitaani (Wamachinga) wakijiandaa kupambana na askari wa kutuliza ghasia (FFU) walipokuwa wakitawanywa na askari hao wakati walipofika katika Ofisi za Kata ya Sinde na Uyole kwa lengo la kuziharibu ofisi hizo kwa kile walichodai hazifanyi kazi ipasavyo na kuwasababishia usumbufu wa mara kwa mara na Polisi kutokana na watendaji hao kutojadi kazi zao zaidi ya kujadi ushuru wanaokusanya.
  Polisi wa kutuliza ghasia wakijaribu Kuzuia Ghasia katika eneo hilo na kufukuza Wamachinga kwa kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.
 Baadhi ya machinga na raia waliokuwa karibu na eneo la tukio wakitimua mbio kujihami na mabomu hayo.
  Baadhi ya Machinga na raia wakiwa mbali na eneo la tukio baada ya kutimua mbio.
Watu mbalimbali wakitimua mbio ili kujiokoa na hatari katika eneo hilo. Picha zote na Latestnews Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages