Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki
(CECAFA) Nicolas Musonye (kulia), akipokea mfano wa cheki yenye thamani
ya shilingi milioni 823 kutoka kwa Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni
ya bia ya Serengeti (SBL) katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya
New Africa jijini Dar es salaam asubuhi hii, katikati ni Jaji Mark
Bomani Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti
(SBL).
Mwenyekiti
wa CECAFA na Rais wa TFF, Leodger Tenga akifafanua jambo mapema leo
asubuhi mbele ya wanahabari kuhusiana na ushiriki wa timu mbalimbali
katika mashindano ya CECAFA Tusker Challange Cup 2011,Tenga amezitaja
timu zitakazoshiriki mwaka huu kuwa ni kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia,Ethiopia,
Sudan, Tanzania, Zanzibar, Eritrea.Tenga aliongeza kuwa kwa kiasi
hicho cha udhamini, kampuni ya bia ya Serengeti inapata heshima ya kuwa
mdhamini mkuu na kupata haki miliki ya kutumia nafasi hii kutangaza
bidhaa ya Tusker kipindi chote cha mashindano haya.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano wa (CECAFA) wakati alipotangaza
udhamini wa shilingi milioni 823 kwa
ajili ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2011 yatakayofanyika
jijini Dar es salaam hivi karibuni, wanaofuatia katika picha ni Teddy
Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) na Ritah Mchaki Meneja wa
kinywaji cha Tusker.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano (SBL),Teddy Mapunda akizungumza leo asubuhi kuhusiana
na kutanganza udhamini wao wa kombe la mashindano ya CECAFA Tusker
Challange Cup 2011 mwaka huu,kupitia
bia yake ya Tusker,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Richard
Wells.Teddy aliongeza kuwa Udhamini huu ni wa kiasi cha fedha za
kitanzania shillingi milioni 823. Fedha hizi zitagharamia mahitaji
kama vile: tiketi za ndege kwa msafara wote wa CECAFA pamoja na
wahusika wakuu wa CECAFA, malazi, usafiri wa magari hapa nchini, watoa
huduma, fedha za washindi, malipo ya CECAFA ndani na nje ya nchi. Kodi
ya uwanja wa mpira, ulinzi na sehemu za mazoezi kwa wachezaji. Hali
kadhalika, fedha hizi zitatumika kuratibu waandishi wa habari na
mahitaji mengine ya utawala. Mashindano haya yanategemewa kuanza tarehe
25 Ocktoba hadi tarehe 10 Disemba 2011.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)