Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma SOCIOLOGY CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) yatoa salam za Rambirambi kwa Wanafunzi Wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma SOCIOLOGY CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) yatoa salam za Rambirambi kwa Wanafunzi Wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma

THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION (UDOMSSO) 

Kwa niaba ya Jumuiya ya Wanafunzi Wanaosoma Shahada Ya Kwanza Ya Sosholojia (Bachelor Of Arts in Sociology) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma   inapenda kutoa pole kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma, Uongozi Wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma, Wanafunzi Wa Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kwa ujumla Kwa Msiba uliotukuta wa Ndugu yetu Yohana Raphael aliyekua Mwanafunzi Wa Mwaka wa 3 wa Shahada ya Kwanza Ya Elimu 

Wanafunzi tunaosoma Shahada ya Kwanza Chuo Kikuu Cha Dodoma Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambi Rambi Kwa Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na Wanafunzi Wa UDOM wote Kufuatia Msiba ulioikumba Chuo Chetu Cha UDOM Kwa kuondokewa na Ndugu yetu YOHANA RAPHAEL aliyefariki ghafla jana katika zahanati ya Chuo Kikuu Cha Dodoma iliyopo Katika Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha 

Vilevile Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambirambi Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki ambao wamempoteza Jamaa,Ndugu, Marafiki yao

Wanafunzi Wote Tunaosoma Shahada ya Kwanza Ya Sociology na Shahada Nyingine Za Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) tunaungana na Wanafunzi Wenzetu Wa Kitivo Cha Elimu kwa pamoja katika wakati huu mgumu wa msiba wa ndugu  yetu YOHANA RAPHAEL

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pepa Peponi Amina na Mungu Awabariki Na Kutujaza Nguvu Ndugu, Jamaa na Marafiki Kwa Kumpoteza Mpendwa Wetu YOHANA RAPHAEL

  Imetolewa Na

LUKAZA JOSEPHAT

AFISA UHUSIANO 

THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO)  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages