Marian Ntuah Picking her T Shirt she won
during Castle Lager's Premier League Perfect Moment Promotion.
Premier League Fans Playing Games During
Launch of Castle Lager's Perfect Moment Premier League Promotion.
--
Castle Lager inadhamini kuonyeshwa kwa
michuano ya ligi kuu ya uingereza ya Barclays kwenye vituo vya luninga
katika nchi 48 barani Afrika. Shuhudia bia yako ya Castle ikionyesha
klabu kubwa za ulaya zikichuana live, wachezaji bora na kukuacha
ukishangilia timu uipendayo.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Castle
Lager kudhamini kuonyeshwa live kwa michuano hii ya ligi kuu ya barani
ulaya katika vituo vya luninga barani Afrika.
Ni sehemu ya
kusaidia uendeshwaji matukio ya michezo katika bara zima na kufanya kila muda kuwa muafaka -
hata kama utatazama michuano hii ukiwa nyumbani na rafiki zako kadhaa.
Mashabiki wapenzi wa soka watapata
nafasi ya kuangalia timu nne zenye kiwango cha juu. Timu hizo ni kama
Manchester United, Liverpool,
Chelsea na Arsenal zitachuana katika ligi kuu ya Uingereza ya Barclays
kila jumamosi katika michuano hiyo itakayoendelea.
Bia yako ya
Castle imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika soka kwa kipindi cha zaidi
ya miaka 30 ikiwa inadhamini Baraza la chama cha soka cha Afrika ya
kusini (COSAFA) Michuano mkubwa, Kombe la Kagame Castle Tanzania na ligi kuu maarufu
ya Soka nchini Afrika ya kusini.
Meneja wa kinywaji cha
Castle Lager, Bi Kabula anasema “Castle Lager kwa makusudi imechagua
vituo vingi vya luninga vitakavyosaidia michuano kuonwa na watazamaji
wengi zaidi.
Amesema pia “kujihusisha
kwa kinywaji cha Castle Lager katika kudhamini mpira wa miguu inatokana
na wao kutambua mapenzi ya wateja wao”. “Tukiwa tunashirikiana na
michuano hii ya ligi kuu ya Uingereza tunakiweka kinywaji chetu katika
sehemu nzuri barani Afrika,” Alisema.
Bi. Kabula anasema pia
kwamba Castle Lager ina mipango ya kuanziasha vitu vya kusisimua zaidi
mwaka huu. “Kwahiyo iwe utatazamia michuano hii katika baa uipendayo au
nyumbani ukiwa unachoma nyama na marafiki zako, hakikisha kila tukio linakuwa la uhakika
ukiwa na Castle Lager yako mkononi. Bia yenye ladha kamili
itakayokuwanya ukate kiu yako."
Kama sehemu ya mipango hii,
Castle Lager pia imezindua promosheni ambayo itawawezesha wateja wa
Castle Lager kujishindia zawadi mbalimbali wakienda kwenye baa au
watakaponunua chupa ya Castle Lager.
Baa
maalum zitakuwa na mabango ya Castle Lager yakiwa na namba maalum za
kuscan. Wateja wataweza kuscan namba hizo kwa kutumia simu zao za
mkononi, ambazo tovuti ya www.theperfectmoment.mobi itafunguka na
kuwawezesha kucheza mpira wa miguu ndani ya tovuti hiyo na
kujishindia zawadi mbalimbali.
Wateja
ambao pia watanunua Castle Lager bia katika baa watapatiwa kadi ambayo
ina namba maalum ambayo wataweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba fulani
na kujishindia zawadi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)