JAJI BOMANI ATAKA MATUMIZI BORA YA URANIUM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JAJI BOMANI ATAKA MATUMIZI BORA YA URANIUM

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

WATAALAMU na wadau mbalimbali wa madini ya urani (URANIUM) wametakiwa kutathimini matumizi bora ya madini hayo kwa manufaa ya nchini. Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mstaafu Mark Bomani, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la urani uliofanyika kwenye hoteli Hyatt Kilimanjaro jijiini Dares Slaam, ambaye alikuwa mgeni rasmi.
“Madini haya ni muhimu yapo sana hapa Tanzania yanaweza kutumika kuzalisha nishati ya umeme. Unapozungumzia lazima uwe unajua manufaa na thari zake na upimwe kipi kinazidi kingine . Hapa kuna wadau mbalimbali watu wanatoka katika kampuni zinachimba madini , wapo wanaweza kusaidia katika kongmano ili kutoa taarifa.
 
“Kabla ya kuamua kuyachimba tujue manufaa kuchimba ni kuuza nje ya nchi au kuzalisha umeme,” alisema Jaji Bomani. Alisema katika suala hilo ni muhimu kuwa na taarifa zinazotosheleza, hivyo alishauri kuwa kusiwe na pupa juu ya uchimbaji wa madini hayo. Naye Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Swaleh Kasela, alisema kuna haja ya serikali kuwaelimisha wananchi ni ya umchimbaji wa madini hayo ni kwa manufaa ya wananchi na iwaondoe hofu kuwa matumizi hayana madhara, kwani yanayotokea ni ya bahati mbaya.

“Ni lazima tujiandae kuwa na wataalumu wetu, ambapo kumwandaa mtaalamu mmoja inachukua zaidi ya miaka 10 yakiwepomafunzo ya kutosheleza,” alisema Kasela. Mhandisi Godwin Nyelo ambaye ni Meneja na mtaalamu wa madini kutoka kampuni ya Uranex aliongeza kuwa madini hayo si hatari kama watu wanavyodhania , bali hatari yake ipo kwenye hatua za utengenezaji.

Aidha alifafanua kuwa watu wa Manyoni wanatumia maji yaliyochanganyika na urani na hawaja pata madhara , hivyo madhara yake yanaonekana iwapo atakuwa ametumia kiwango kikubwa cha madini hayo. Hata hivyo alishauri kuna haja ya kufanyika utafiti kwa watu wa manyoni wanaotumia maji hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nantumbo, Saveli Makatta aliwataka wawekezaji kuja kuweza kwa kuwa tayari miundombinu imeshaanza kuboreshwa.

Mtaalamu mwingine kutoka kampuni ya Uranium One, ambaye ni Meneja Mwakilishimkazi, Asa Mwaipopo ,alisema kongamnao hilo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, taasisi za madini na wataalamu kutoka Afrika Kusini. Madhumuni yake ni kushiriki katika mjadala ili nchi wakati nchi inaelejea katika uchimbaji wa madini hayo, hivyo matumizi yake ni yatakuwa kwa ajili ya kutoa nishati ya umeme pekee.

Alizitaja nchi ya Namibia kuwa ndio inaongoza katika uchimbaji wa madini hayo barani Afrika  ,ikifuatiwa na Niger na Afrika Kusini. Aliongeza kuwa Tanzania itaanza kuchimba madini hayo mwaka 2013, hivyo inaweza kushika nafasi ya tatu kwa kuzalisha madini hayo kwa wingi katika bara hilo, wakati kidunia kuwa ya nane.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages