Sauda Simba muusika mkuu katika Filamu ya CPU |
Director wa Filamu ya CPU Karabani akitoa maelezo na Steven Sandhu muusika mkuu katika filamu ya CPU |
Evans Bukuku
akionyesha Poster ya Filamu ya CPU
--
Ile filamu ya
C.P.U ambayo imekuwa ikisubiriwa na Watu wengi hatimaye mwisho wa wiki
hii itaweza kuzinduliwa na kuoneshwa rasmi kwa wapenzi wa tasnia ya
filamu.
Akizungumza
na waandishi wa habari mratibu wa filamu ya C.P.U bwana Evans Bukuku
alisema kuwa “Filamu ya C.P.U kwa mara ya kwanza itaoneshwa hapo
Ijumaa tarehe 25 Novemba 2011 kuanzia saa 1 na dakika 45 jioni
katika ukumbi wa Sinema wa mlimani city century cinemax, kisha
itaendelea kuoneshwa kwa wiki nzima muda kama huo mpaka mnamo tarehe 1
Disemba 2011.
Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa
wapenzi wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla kwenda
kupata kujionea kazi ya ubora wa hali ya juu ambayo imefanyika hapa
Tanzania.Kwa wale watakaopata nafasi ya kuitazama Filamu ya C.P.U hakika
watathibitisha hili.
Akizungumzia kwa ufupi juu ya Filamu hii
Bw. Bukuku alisema, “ filamu ya C.P.U imetengenezwa na kampuni ya Haak
neel kwa ushirikiano na Wegos Works Production ikiwa
imeandikwa na Novatus Nago na kuongozwa na Karabani huku watayarishaji
wakuu wakiwa ni Prof. Martin Muhando na Bw Godfrey Mahendeka. CPU ni
aina ya hadithi ya kipelelezi yaani ‘Investigatory story’ ikiwa inazungumzia
kitengo kilichoundwa kwa ajili ya kufuatilia na kutatua matatizo
yanayowapata watoto. Hivyo Maria Isabela (Sauda Simba) anateuliwa na
serikali kuongoza timu hiyo, katika hilo
inabidi awashawishi watakao msaidia ambao ni Alex Kibera(Nkwabi Juma)
jambazi anayetumikia kifungo cha miaka 30 jela, David Kifati(steven
Sandhu) mtaalamu wa kompyuta na kijana mwenye uelewa mkubwa ambaye
anatoka katika familia bora na anayependa anasa, pia kuna Rehema Mlaki
(Subira Wahure) akiigiza kama msichana anyefanya kazi ya uwakili wa
kujitegemea.
Baada ya kufanikiwa kuwashawishi wanaanza kazi ya kwanza
ambayo kiujumla ni yenye misukosuko na inayohitaji umakini wa hali ya
juu kwa kuwa ni ya hatari sana hasa wanapokabiliana na mtu
kama Jibaba(Mobby Mpambala) mmiliki wa danguro kubwa hapa jiji na
mzoefu wa biashara haramu.hapo ndipo utapata kuona mikiki na ufanisi
uliooneshwa na waagizaji takribani 180. Filamu ya CPU ikiwa imetengezwa
hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti zaidi ya 30.
Lugha
iliyotumika katika filamu hii ni Kiswahili lakini pia lugha ya
kiingereza imetumika kama “subtitles”. Umri wa kutazama filamu
hii ni kuanzia miaka 13.Kiingilio filamu ya C.P.U ni sawa
na kiingilio cha kawaida cha Century Cinemax
Mpaka
kufanikisha tukio hili tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono tangu
mwanzo, East Africa Radio na East Africa Television,
I-Noch Company Limited , waandishi wahabari wote kwa ujumla , baadhi ya
Taasisi za kiserikali, mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali hasa
yanayohusika na masuala ya watoto na watu mbali mbali.
Unaweza
kuanza kufanya booking ya Ticket yako kuanzia sasa kupitia namba
0715 246362
0753 246362
Kwa
maelezo na taarifa zaidi juu ya filamu ya CPU unaweza kupata kupitia
vyombo mbali mbali vya habari pia unaweza kufuatilia zaidi kupitia
tovuti ya www.cpu.co.tz
au www.filamucentral.co.tz
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)