Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya (kulia)
akizungumza katika warsha ya wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali
walipokutana kujadili vitendo vya Unyanyasaji wa Kijinsia jijini Dar es
Salaam Novemba 23, 2011.
Baadhi ya wahariri wa habari
kutoka vyombo anuai nchini Tanzania walipokutana Novema 23, 2011 kwenye
semina kujadili masuala ya Ukatili wa Kijinsia, semina hiyo iliandaliwa
na TAMWA kwa kushirikiana na UNFPA.Picha na MpigaPicha Wetu
---
---
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA) jana kimewakutanisha wahariri kutoka vyombo mbalimbali
vya habari nchini kujadili ukatili wa kijinsia kwa jamii.
Hatua hii ni moja ya programu ya
Kihistoria ya Siku 16 za wanaharakati kupinga ukatili wa kijinsia kwa
jamii ambayo ilianzishwa tangu mwaka 1991 na Kituo cha Kimataifa cha
Wanawake katika Uongozi (Centre for Women’s Global Leadership).
Akizungumza katika semina hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya amesema lengo la semina kwa
wahariri hao ni kuhakikisha wanafahamu mchango wa wanaume katika
kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Tanzania.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo alisema
lengo lingine ni kuhakikisha wahariri wanakuwa mstari wa mbele kuanzia
Novemba 23 hadi Desemba 10 kuwaamsha kiutendaji pande husika kuchukua
hatua juu ya vitendo hivyo vya kikatili.
Aidha mada anuai zimetolewa kwa
washiriki ili kujenga uelewa juu ya namna ya kutumia nafasi zao kwa
vyombo vya habari na kuleta mabadiliko katika suala zima la ukatili wa
kijinsia ambalo limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na wanafunzi hasa
wa kike.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga
Ukatili wa Kijinsia ni “Miaka 50 ya Uhuru: Pinga Ukatili Kuimarisha
Tanzania Huru”.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)