Dk Willbroad Slaa na Tundu Lissu Wapandishwa Kizimbani Mkoani Arusha - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Dk Willbroad Slaa na Tundu Lissu Wapandishwa Kizimbani Mkoani Arusha


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa, akishuka kutoka kwenye Karandinga la Polisi, kusomewa mashitaka yanayomkabili na washitakiwa wengine 26 waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume na sheria.
--
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na wanachama wengine 25 wa chama hicho wamekamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.Mbali na hao, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ametakiwa kujisalimisha mwenyewe polisi baada ya kutoweka katika Viwanja vya NMC Unga Limited baada ya polisi kufanya operesheni ya kushtukiza kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama hicho na viongozi wao waliokesha hapo usiku wa kuamkia jana.

Juzi, viongozi hao wa juu wa Chadema walitangaza kupiga kambi kwenye viwanja hivyo kwa siku tatu ikiwa ni shinikizo la kutaka mahakama itoe kibali maalumu cha kumtoa gerezani Kisongo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye naye anatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali.

Wengine waliofikishwa mahakamani pamoja na Dk.Slaa kuhusu mashitaka hayo  ni Tundu Lissu,David Godfrey (18), Ally Hussein (20), Frank Chami (24), Stella Mushi (21), Francis Smweli (20), Paulo Meena (18), Beatrice John (28), Matei Thobias (38), Davies Sedeka (29) na Wilson Andrea (24).
 
Wengine ni Richad Urasa (27), Abubakar Mrema (25), Peter Davis (14), Proches Blacy (36), John Msaki (53), Stephano Swai (33), Mohamed Mhoji (21),Titus Urio (30), Nelson Kimario (23), Meshack Beture (23) na Jimmy Evarist (22.)Kwa habari zaidi bofya Hapa na Hapa na Hapa....>>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages