TIMU ya soka ya Kumasi Asante kotoko ya Ghana
inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki
dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa
Taifa.Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya
Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa
mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.Masanja
alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam
kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya
Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.
Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya
timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya
Tanzania Bara msimu huu.Aliongeza kuwamakocha wawili, mkongwe, Abdallah “KingMputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi
la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo
baadaye. Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari
wa timu, Juma Sufiani.Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa
wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo
watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.Masanja alisema kuwa Yanga na Simba
zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane
mwaka 1935. Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja
kuanzia mwa 1922.Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo
itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa
zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida
mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.Wakati Nchunga akisema hayo,
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija
kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja
kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Alisema
kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na
kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)
Lukaza Blog is a resources blog providing high quality articles with premium topics and well drafted. The main mission of Lukaza Blog is to provide the best quality articles which are relevance, original, truth and education materials designed and perfectlly to deliver best result for your knowledge and understanding of new things.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua...
Contact Form
About Me
Hello, my name is Josephat Lukaza. I've 12 years in Blogging and An Award Winner for the BEST Political Blog in African Bloggers Awards in 2015 Learn More →
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)