Wakazi
wa kata ya Iyela mtaa wa Airport wakifanya jitihada za kuokoa maisha
ya Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Igale
wilayani Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa na mauti wakati
akichimba kisima chenye futi 96 kipenyo cha futi 2.
Licha
ya juhudi za wakazi wa kata ya Iyela mtaa wa Air Port jijini Mbeya
kujaribu kuokoa maisha ya Fraida Mwashozya mwenye umri wa miaka 25 mkazi
wa kijiji cha Igale wilayani Mbozi, zimegongwa mwamba baada ya kufikwa
na mauti.
Juhudi
hizo zilifikia kikomo majira ya saa 11 jioni pale mwli wake
ulipoibuliwa kutoka katika kisima hicho akiwa amefariki, juhudi za
uokozi zilianza majira ya asubuhi kuanzia saa moja na dakika arobaini na
tano ambapo marehemu mbaye alikuwa akichimba kisima chenye urefu wa
futi 96 na kipenyo cha mzunguko futi 2 kazi iliyofanyia kwa siku moja
wakati akitaka kumridhisha mwajiri wake aliyemwagiza kukichimba kisima
hicho.
Inaelezwa
kuwa Fraida Mwashozya na mwenzake Nesco Mwamlima mwenye umri wa miaka
23 walipewa ajira ya kuchimba kisima chenye urefu wa futi 96 bwana
Piusi Simchimba mwenye umri wa miaka 64 kwa ujira wa shilingi elfu 55
ambapo baada ya kumaliza waliambiwa hawatoweza kulipwa hadi watakapo
ongeza urefu wa kisima hicho.
Tukio
hilo la kutumbukia kwa Fraida limetokea jana majira ya saa moja za
asubuhi lakini Jeshi la polisi, kikosi cha uokoaji na wakazi wa eneo
hilo wameshindwa kumuokoa na kwamba jitihada za kutumia watu kuingia
kisimani humo zimeshindikana kutokana na kukosekana kwa hewa kisimani
humo.
Aidha
watu wawili Nesco Mwamlima na Juma Mwanyeyere walipojaribu kuingia
kwenye kisima hicho kumuokoa nao walishindwa kutokana na kuhishiwa hewa
lakini wao waliokolewa na afya zao zinaendelea vizuri.
Afisa
mtenda wa kata ya Iyela Ezekiel Kipako amesema zoezi la uokoaji
limemalizika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Mbeya.Picha na Habari Kwa Hisani Ya Mbeya Yetu Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)