
Waziri
wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernald Membe akizungumza
katika maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara
hiyo yaliyofanyika jana, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuhudhuriwa
na wafanyakazi pamoja na mabalozi wastaafu mbalimbali.

Mfanyakzi
bora wa jumla katika wizara ya mambo ya nje Bw.Seif Kondo kulia
kutoka kitengo cha habari akipokea cheti cha ufanya kazi bora kutoka
kwa Waziri Bernald Membe.

Waziri Bernald Membe akimkabidhi cheti cha ufanyakazi bora Grace Mjuma Kaimu mkurugenzi Idara ya Mawasiliano ya Kikanda.

Waziri
Bernald Membe wa tatu kutoka kulia akiwa amekaa meza kuu pamoja na
mabalozi wastaafu walioshiriki katika maadhimisho hayo.

Kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam likitumbuiza katika maadhimisho hayo

Wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya nje wakishiriki katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara hiyo.

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo viwanja vya Mnazi Mmoja jana.

Wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya nje wakishiriki katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania katika wizara hiyo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)