WIZARA YA MAJI YAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU KWA MAONYESHO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WIZARA YA MAJI YAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU KWA MAONYESHO

Mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa Maji kilichopo Ubungo jijini Dares Salaam, Adam Massam akiwaonesha baadhi ya wananchi teknolojia ya kuvuna maji ya mvua, ambayo hunaweza kutumia kumwagilia mazao na matumizi mengine leo (jana) wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya Wizara ya Maji.
Naibu Waziri wa Maji, Gerson (kushoto) akimkabidhi tuzo ya utendaji mzuri wa kazi aliyekuwa Waziri wa Maji wa kwanza ambaye pia ni mwanzilishi wa wizara hiyo, Dk. Pius Ng'wandu (kulia) leo (jana) wakati wa ufungaji wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya wizara hiyo.

Naibu Waziri wa Maji, Gerson (kushoto) akibadilishana mawazo na aliyekuwa Waziri wa Maji wa kwanza , ambaye pia ni mwanzilishi wa wizara hiyo, Dk. Pius Ng'wandu (kulia) na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Christopher Sayi leo (jana) wakati wa ufungaji wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya wizara hiyo.
baadhi ya wanachi na watumishi wa Wizara ya Maji wakifuatilia kwa makini maadhimidho ya miaka 50 ya wizara hiyo leo wakati ufungaji wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa Maji kilichopo Ubungo jijini Dares Salaam.
PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages