Mkuu wa mkoa wa Arusha Ameamuru Kukamatwa Mara Moja Kwa AfisaMtendaji wa kata ya Elerai Joackimu Kisarika na Mfanyabiashara,Salim Boy - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mkuu wa mkoa wa Arusha Ameamuru Kukamatwa Mara Moja Kwa AfisaMtendaji wa kata ya Elerai Joackimu Kisarika na Mfanyabiashara,Salim Boy

Mkuu wa mkoa wa Arusha ameamuru kukamatwa kwa AfisaMtendaji wa kata ya Elerai Joackimu Kisarika  na Mfanyabiashara,Salim Boy baada ya kukutwa na kashfa ya kuiba sukari mifuko 127 yenye thamani ya shs 10,795,000 milioni  iliyokuwa itolewa kwa wananchi wakata hiyo.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa mkoa huo kutembelea kata hiyobaada ya kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchikuhusiana na kusuasua kwa ugawaji wa sukari katika kata hiyo. Mulongo aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano  wa watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,madiwani  pamoja na wananchi wa kata ya elerai katika manispaa ya jiji la Arusha.
 
Ambapo Mkuu wa mkoa huo,baada ya kufika katika kata hiyo alibaini kuwepo kwa upotevu wa sukari hiyo huku ikiwa haijulikani ilipo hadi sasa ndipo alipohoji kujua ukweli wake.
Alisema kuwa, wananchi wa kata hiyo walichanga fedha kwa ajili ya ununuzi wa sukari hiyo na kumteua Mfanyabiashara huyo kuwa ndiye Msimamizi wa fedha hizo, badala yake Mfanyabiashara huyo alienda kinyume na kuchukua sukari hiyo mifuko 127  na kuipeleka
kusikojulikana hali iliyozua mtafaruku mkubwa katika kata hiyo na hivyo kuhitaji msaada wa Mkuu wa mkoa.
 
Aidha baada ya Mkuu wa mkoa kumhoji , mfanyabiashara huyo alijibu kuwa yeye huwa anakusanya fedha na kisha kumkabithi Afisa Mtendaji huyo na hivyo ndicho alichokifanya siku hiyo. Hata hivyo, Afisa Mtendaji huyo alipohojiwa alisema kuwa, siku hiyo
hakuwepo katika shughuli hiyo na wala hajui chochote kinachoendelea kuhusiana na upotevu huo Kufuatia mahojiano hayo ya muda mrefu kati ya Mkuu wa mkoa,Mfanyabiashara  na Afisa mtendaji wa kata hiyo, ndipo Mkuu wa mkoa aliamuru askari wa jeshi la polisi kuwakamata na kuwaweka ndani kwa pamoja ili wakajibu mashitaka hayo na pindi uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani. 
 
Mulongo, kutokana na tabia hiyo alikasirishwa sana na kuwaonya maafisa watendaji na wafanyabiashara ambao  wamepewa dhamana ya kusimamia wananchi na kuwaongoza kwa ukweli na uaminifu badala yake wamekuwa wakikiuka na kudhulumu haki za wananchi hao.
'Mimi nitahakikisha nimekula sahani moja na watendaji wasio waaminifu, na nitahakikisha nimemfukuza mmoja baada ya mwingine hadi mkoa wetu ukae kwenye mstari ulionyooka, na kamwe sitavumilia kufanya kazi na viongozi kama hawa katika mkoa wangu 'alisema Mulongo.
 
Aidha Mulongo alisema, kutokana na hali hiyo ni lazima njia mbadala itumike ili wananchi wapae sukari kwa wakati na kwa bei elekezi ambapo amewataka wananchi wachaguane na kuteua mwenyekiti na zoezi zima walifanye wao na viongozi wa vijiji kazi yao kubwa ni kusimamia nakuhakikisha wananchi wanapata sukari.
 
Pia aliwataka viongozi kuacha siasa ambazo zimekuwa zikiingizwa hata kwenye mambo ya jamii bali watatue matatizo ya wananchi na watoe huduma kwa wananchi kwa kufuata miiko ya kazi yao inavyosema kwa kuheshimiana bila kujali elimu,wala itikadi za chama.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages