Kikosi cha Zima Moto kikipambana na moto huo.
DUKA la vifaa vya ujenzi na umeme lililopo jirani na Benki ya Afrika (BOA) mtaa wa Madaraka katikati ya mji wa Morogoro linalomilikiwa na Mtanzania mwenye asili ya India aliyefahamika kwa jina moja la Seif, leo mchana limeteketea kwa moto wakati mmiliki wa duka hilo akiwa msikitini kuswali sala ya ljumaa.
Bw. Seif alipata taarifa hizo kwa njia ya simu akiwa msikitini na kufika eneo la tukio akiwa amesindikizwa na wafanyabiashara wenzake kuja kushuhudia duka lake lililokuwa linateketea kwa moto.
Watu walioshuhudia tukio hilo ambao wanafanya biashara jirani na duka hilo, walidai kwamba walishangaa kuona moshi mzito ukitoka ndani ya duka hilo wakati likiwa limefungwa.
"Mzee Seif alikuwa msikitini akiswali sala ya Ijumaa wakati huku duka lake likiteketea kwa moto kama unavyoona, tunahisi moto huu umesababishwa na shoti ya umeme, baada ya kuona hali hiyo tulimpigia simu mzee Seif ambapo alifika hapa na wenzake aliokuwa akiswali nao" alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hamis.
Kufuatia kufungwa kwa mlango wa duka hilo, Kikosi cha Zima Moto kiliamua kulivunja duka hilo kwa lengo la kupata nafasi ya kuingia ndani na kuzima moto huo japo zoezi hilo lilichukua muda mrefu na kusababisha vitu vingi kuteketea kwa moto kwenye duka hilo.

PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE/ GPL, MOROGORO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)