Wadau
picha hizi zinatisha lakini mtuwie radhi kwani ndiyo hali halisi
iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Tabata na hakuna mtu anayeweza
kuvumilia maovu haya yanaofanywa na watu wasiokuwa na utu.
Leo saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa
anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani (kama picha zinavyooneka hapo juu).
Bwana Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi yalipofika nyumbani kwa bawana Mwakyusa yalimjeruhi
kwa shoka bwana mussa na,
wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea kufungua
spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana Mwakyusa
alishtuka na ndipo majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha Mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa mahututi. bwana. Jumaa Almasi afisa uhusiano
mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli bwana Mussa
amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)