UVCCM WAZINDUA MATAWI YA CCM ARUSHA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UVCCM WAZINDUA MATAWI YA CCM ARUSHA.

Kaimu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM taifa (UVCCM),Benno Malisa akifungua tawi la chama hicho eneo la Majengo juzi wakati wa ziara ya uzinduzi wa matawi ya chama hicho wilayani Arusha,pembeni yake kushoto ni mbunge wa viti maalumu kupitia umoja huo mkoani Arusha,Cathwrine Magige.
Mbunge wa viti maalumu kupitia UVCCM mkoani Arusha,Catherine Magige akiwapungia mikono wafuasi wa umoja huo nje ya jengo la makao makuu ya chama hicho mkoani Arusha wakati wa ziara ya uzinduzi wa matawi ya chama hicho wilayani Arusha,zaidi ya matawi 20 ya chama hicho yalifunguliwa katika sehemu mbalimbali.
Kaimu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) ngazi ya taifa,Benno Malisa akizungumza na wafuasi wa umoja huo nje ya jengo la makao makuu ya umoja huo mkoani Arusha juzi kabla ya ziara ya uzinduzi wa matawi mbalimbali ya chama hicho mjini hapa,pembeni yake ni mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha,James Ole Milya(pich zote na moses mashalla)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages