Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu anaezidi kushusha neema zake. Pili kwa heshima
kubwa napenda kuwasalimu wadau wote wa Blog Tanzania na Duniani kwa ujumla.
kubwa napenda kuwasalimu wadau wote wa Blog Tanzania na Duniani kwa ujumla.
Napenda kuchukua nafasi hii adimu ya kuweza kuitambulisha Blog Mpya kabisa nchini kwa wadau na hasa Wanafunzi wote wa elimu ya juu inayojihusisha na utafutaji na ukusanyaji wa habari zinazowahusu wanafunzi wa Vyuo vikuu nchini na Tassisi zote za Elimu ya juu. Wanafunzi wote na wadau wote wa Elimu nchini watakuwa na fursa ya kufikisha habari, taarifa na maoni kwa jamii nzima ya vyuo vikuu nchini.
Blog hiyo inajulikana kama www.tzcampusvibe.wordpress.com inatoa habari zote zinazomhusu mwanafunzi wa chuo kikuu, iwe ya kijamii, kimasomo, kiuchumi , kisiasa ama hata kiburudani ili mradi inahusu jamii ya elimu ya juu nchini
na hata nje ya nchi lakini ni mwanafunzi wa kitanzania.
Karibuni sana wadau katika Blog yenu hii mpya kujua michakato mizima inayotokea taasisi za Elimu ya juu nchini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)