Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini mjini Mbeya
Jengo la TCI Mkoani Mbeya
Akizindua
ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo
ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya
Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Mbilinyi alisema Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkaribisha waziri Mary Nagu
alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la
Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii
katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika
eneo la Kiwira.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji
jijini Mbeya kutoka Kushoto Mbele ni Mrs Kadyanji na anaefuatia ni Mrs.
Yunge na wajasilia mali wengine.Picha zote na Mbeya yetu Blog





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)