SALAM,
Napenda
kutoa shukurani zangu za pekee kwa Mwenyezi Mungu, Familia yangu,
Marafiki zangu, mashabiki wangu, wadau na watanzania wote kwa ujumla
walioweza kunipigia kura ambazo zimefanikisha blog ya MissJestinaGeorge kuibuka
kidedea na kunyakua ushindi mkubwa wa kuwa ''BLOG BORA YA MWAKA
2011'' katika tuzo za BEFFTA zilizofanyika nchini UK mapema wiki
iliyopita.
Mchakato
mzima wa kumtafuta mshindi ulikuwa na changamoto lukuki ukizingatia ya
kwamba kulikuwa na jumla ya blogs 15 za kimataifa kutoka nchi
mbali mbali Duniani. Kutokana na ushirikiano wenu mzuri mmeiwezesha
blogu yetu kupata ushindi mnono na vile vile kunipatia fursa nzuri ya
kuiwakilisha vyema Tanzania Ughaibuni.
Ni
vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa mchango wenu uliosadia
kuwezesha blog yetu kunyakua ushindi mkubwa ingawa ningependa
kuwatambua wafuatao: kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu zote za
dhati kwa timu ya URBAN PULSE CREATIVE kwa mchango wao mkubwa waliotoa, wanachama wenzangu wa AMTTA (Amka Mwanamke Twende Tujikomboe Afrika) kwa kuwa na mimi bega kwa bega nawapenda sana. Pia natoa shukrani kwa Bloggers wenzangu wote, tovuti mbalimbali, TONE RADIO popote pale walipo kwa michango yenu.
Nawasihi sana tuendelee kushikamana, kupendana
na Kusaidiana kwa hali na mali ili isiwe tu kuleta maendeleo nchini
kwetu bali pia kupeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania Duniani kote.
Napenda kuitoa wakfu tuzo hii kwa dada yangu mpendwa Kissa George aliyetutoka ''I miss you so much Sis'' najua kama angekuwa hai angefurahia sana.
Napenda kuitoa wakfu tuzo hii kwa dada yangu mpendwa Kissa George aliyetutoka ''I miss you so much Sis'' najua kama angekuwa hai angefurahia sana.
Mwisho
namshukuru sana binti yangu Iman ambae amekuwa nguzo na muhumili
mkubwa katika maisha yangu kwa kunipatia nguvu za kuendelea mbele siku
hadi siku. Binadamu kushukuru ni wito ila leo umekuwa ni wajibu wangu.
Asanteni sana,
Mungu awabariki sana na ninawapenda sana
Jestina George






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)