Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa
Geti kuu la kuingia Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.
Wanachuo hao hapa wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.
Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.
Ni
jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa
Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa
umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika
nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila
hitimisho la mgomo huu.
Kwa
kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana
ya kusimamia na kuongoza ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi
ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti
na vyuo vingine vya binafsi (private).
Sisi
kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na
Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara
ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student
Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu.
Pesa
nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha
wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili
tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa
letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)