Rais
Dk. Jakaya Kikwete akisaliaiana na Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda, mara
baada ya kuwasilia katika uwanja wa ndege wa Mpanda leo asubuhi, tayari
kwa kufungua mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanzaganyika
mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma unaohudhuriwa na Mabalozi, maofisa wa
serikali na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji wa ndani na wa nje ya
nchi, mkutano huo hivi sasa unaendelea kwenye ukumbi wa idara ya maji
mjini Mpanda. Mpaka sasa Rais tayari ameshaingia ukumbini na anaendelea
na hotuba yake ya ufunguzi matukio zaidi ya ufunguzi wa mkutano huo
yatawajia baada ya muda, katika picha kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa
mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Rais
Jakaya Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa mkoa
wa Rukwa Injini Stella Manyanya, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Mpanda.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi pamoja na wawekezaji wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Picha na habari kwa hisani ya http://fullshangwe.blogspot.com/








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)