NBC yaandaa tafrija kwa wadau na wanachama wa Mfuko wa PPF - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NBC yaandaa tafrija kwa wadau na wanachama wa Mfuko wa PPF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma William Erio (katikati) akishikana mikono na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Mwinda Kiula-Mfugale wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni, Minnie Kibuta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio (kulia) akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko-Simba wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa PPF, Bi. Lulu Melenge.
Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na NBC kwa wadau wa PPF mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wadau wa PPF wakifurahia vinywaji katika hafla hiyo pembeni ya jiko la moto lililowekwa kwa ajili ya hali ya hewa ya kibaridi iliyopo mjini Arusha kwa sasa.
Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta (kushoto) akimsevu chakula Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wadau na wanachama wa PPF waliokuwa katika mkutano wao mjini
Arusha mwishoni mwa wiki
 Kikundi cha wamasai kikitoa burudani katika hafla hiyo.
 Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) Ofisa Uhusiano, Eddie Mhina na mdau wa PPF Muhidini Michuzi wa Globu ya Jamii wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo mjini Arusha mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages