Gari la kubeba mafuta kama lilivyokutwa likihakikiwa vipimo vyake katika karakana na Wakala wa Vipimo na Mizani.
Meneja wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw Hamisi Hamidu (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu ( Mwenye suti katikati) katika ziara yake Jijini Dar es salaam
Meneja wa Vipimo Mkoa wa Ilala Bw Hamisi Hamidu (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu ( Mwenye suti katikati) katika ziara yake Jijini Dar es salaam
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu( Aliechuchumaa
kulia) na Meneja wa Vipimo na Mizani Mkoa wa Ilala Bw Hamisi Hamidu
(kushoto) wakiangalia kipimo cha kutambua usahihi wa mafuta yanayopita
katika pampu za kuuzia bidhaa hiyo.Wanaotazama ni maafisa wa Wakala
wa Vipimo na Mizani na wenzao kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aina mbali mbali za mizani zinazotumika katika kupima uzito wa bidhaa.
Picha
ya pamoja ya wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo na Mizani na Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Aliekaa katikati)
mara baada ya ziara yake kuwatembelea.
....
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu,jana ametembelea
taasisi ya Wakala wa Vipimo na Mizani iliyo chini ya Wizara yake ili
kuonana na wafanyakazi na kujionea baadhi ya shughuli zao.
Naibu
Waziri Nyalandu amepokelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo
Bwana Deo Maneno na kupewa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo ambayo
imeonesha mafanikio makubwa katika kulinda haki za watumiaji hasa
wakulima dhidi ya vipimo batili.
Akizungumza
na Wafanyakazi na Vyombo vya habari mara baada ya ziara yake, Mh
Nyalandu ameitaka taasisi hiyo kuongeza juhudi katika kudhibiti vipimo
ili kuhakikiksha kuwa, watumiaji wanapata bidhaa na huduma
zinazolingana na thanmani ya fedha wanazotoa.
Ameahidi
kuusaidia Wakala huo ili kupata sheria mpya yenye nguvu zaidi kuliko
ilivyo sasa ambapo wakosaji huamriwa kulipa faini ndogo zinazowafanya
kuendelea kutumia vipimo batili bila wasiwasi wowote.
“
Kazi yenu ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa, watu wa kada zote
wanawategemea katika kupata haki.. Kuanzia wakulima mpaka wanunuzi wa
bidhaa za viwandani, wote wanataka vipimo sahihi,pigeni vita kangomba
na lumbesa, shirikianeni na mamlaka nyingine kutimiza wajibu huu,
wajengeeni watumishi wenu mazingira bora ya kazi, mtafanikiwa kuliko
ilivyo sasa”, amesema Nyalandu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)