Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Tanzania Distillers Limited (TDL) Ijumaa itafanya bonanza la
kumzawadia mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Gurumo katika viwanja
vya Leaders Club.
Mratibu
wa tamasha hilo, Mohamed Pizzaro alisema jana kuwa maandalizi ya
tamasha hilo yamekamilika na mkurugenzi mtendaji wa TDL, David Mgwasa
ndiye atakayetoa tuzo hiyo kwa Gurumo kama sehemu yake kuadhimisha
miaka 50 ya Uhuru.
Pizzaro
alisema kuwa Gurumo alianza muziki miaka ya 50, lakini alianza rasmi
muziki wa jukwaani mwaka 1961 akiwa na bendi ya Kilimanjaro Chacha
ambapo mwaka 1963, akajiunga na Kilwa Jazz.
Alisema
kuwa baada ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wafanyakazi (NUTA), Gurumo
akawa mwanamuziki wa kwanza kujiunga na bendi hiyo ambayo alidumu nayo
mpaka mwaka 1978 alipojiunga na DDC Mlimani Park ‘Wana Sikinde Ngoma ya
Ukae’ ambayo alihama mwaka 1986 na kujiunga na Orchestra Safari Sound
(OSS)‘Wana Ndekule’.
Alifafanua kuwa Gurumo alirejea Msondo mwaka 1990 ambapo tokea ajiunge huko, hajahama tena.
“Zawadi
gani atakayokabidhiwa, hiyo inajua kampuni ya TDL na Mgwasa mwenyewe,
lakini ni ‘surprise’ kwa mashabiki na Gurumo mwenyewe,” alisema
Pizzaro.
Alisema
kuwa shamrashamra za tamasha hilo ambalo pia litakuwa la kumuenzi
marehemu Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere litatumbuizwa na bendi
ya Msondo baada ya mechi mbili za timu za maveterani.
Mechi ya kwanza itakuwa kati ya Kigamboni na Namangan a mechi ya pili itakuwa kati ya Brake Point (BP) na Mango Garden.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)