Marehemu
Rahma Swai (wa kwanza kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wenzake wa shindano la Miss Kanda ya Mashariki
lililofanyika mjini Morogoro.
Rahma
alifariki Okotoba 18,2011 mjini Mtwara baadaya kuugua ghafla na
kupelekwa Hospitali na kufariki wakati akienbdelea na matibabu.
Mwili
wa marehemu uliwasili jana nyumbani kwao Changanyikeni jijini Dar es
Salaam na anataraji kuzikwa kesho mara baadaya kuwasili kwa mama yake
aliyekuwa safarini Nchini Malawi kikazi na anatari kuwasili hii leo.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa Muandaaji wa Shindano la Miss Mtwara 2011,
Rajab Mchata amesema Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania na baadhi ya
warembo wa Kanda ya Mashariki na wale wa Miss Tanzania walifika
kuomboleza msiba huo.
Hadi mauti yanamfika Marehemu Rahma (21) alikuwa ni mfanyakazi wa kituo cha Redio cha SAFARI RADIO FM cha mjini Mtwara.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)