Mbunge
wa Monduli, Edward Lowasa leo amezungumza na waandishi wa Habari
nyumbani kwake Monduli juu ya masula mbalimbali yanayoandikwa katika
vyombo vya habari nchini yakimusisha yeye. Ifuatayo ni hotuba yake
aliyoisoma hii leo.
HOTUBA YA MBUNGE WA MONDULI,EDWARD LOWASA KWA WAANDISHI WA HABARI MONDULI, OKTOBA 19,2011.
NDUGU
wana habari nimewaita katika mkutano huu leo kwa sababu moja kubwa,
kutoa ufafanuzi kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakitokea huku
yakinihusisha mimi binafsi kwa namna ambayo sasa yanatishai ustawi na
mshikamano wa kimaadili, kihistoria na kikazi miongoni mwa viongozi na
baina ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi(CCM).
Ndugu
wana habari, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu habari
zinazoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazolihusisha jina
langu na harakati kadha wa kadha chafu ambazo hata mimi mwenyewe
ninayehusishwa nazo huwa nazisikia na kuzijua baadaya kuwa
zimesharipotiwa katika vyombo vya habari.
Uamuzi
wangu kukutana nanyi leo hauna makusudi ya kuzozana na vyombo vya
habari wala kwenda kinyume na utamaduni wakimaadili wandani ya chama
changu unaaotutaka viongozi kujadili masuala yanayokihusu chama chetu
ndani ya vikao vyetu rasmi vya kimaamuzi bali kutoa ufafanuzi na
angalizo kwa pande zote hizo ambazo zinaguswana matukio yanayoendelea
kutoka leo hii.
Moja
ya mambo ambayo yameligusa jina langu kwa namna hiyo ni lile
linalonihusisha eti na kundi moja la wanasiasa ambao wamekuwa na
mikakati ya kumhujumu mwenyekiti wetu wa chama, Mheshimiwa Rais Jakaya
Kiwete. Hakuna shaka ni madai ya kipuuzi, kizishi na yenye malengo
machafu.
Hawakuishia
hapo sasa wamefikia hatua ya kuvitumia vyombo hivyo hivyo vya habari na
kufikia hatua ya kudai kwamba nimeanza kuandaa orodha ya kile
wanachokiita madhambi ya Rais Kikwete ambayo wanadai nimepanga kuyasoma
wakati wa kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (CCM).
Ninaamini
kwa dhati kabisa kwamba, waandishi wa habari wanaofuatilia kwa karibu
na kwa umakini mwenendo wa masuala ya kisiasa nchini wanatambua kwamba,
watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo
kwa malengo ya kufikirika ya kujisafisha njia kisiasa.
Nijambo
lisiloingia akilini kunihusisha na kile kinachoitwamikakati ya
kumhujumu rais au chama ambacho mimi ni kada wake wa mudamrefu, mbunge
anayetokana na chama hicho hicho na mtu ninayeiongoza Kamati nyeti ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na zaidi ya yote kiongozi wa
ngazi mbalimbali za kisiasa na kiserikali nilizowahi kushika.
Kuhusu hili
napenda kusema kwa uwazi kwamba, mbali ya ukweli kuwa sijapata
kufikiria hata mara moja kuhusu hicho wanachokiita mabaya au madhambi ya
rais, sina na wala siijui hiyo wanayoiita kuwa ni orodha ya mabaya ya
namna yoyote ya Rais Kikwete.
Mbali ya
ukweli kwamba huo ni uongo wa wazi, silica yangu kama mwanasiasa na mtu
mwenye dhamana kubwa kwawatu wa Monduli na kwa taifa langu haiwezi kamwe
kunituma nianze kupanga mikakati ya kumhujumu kiongozi wetu mkuu au
chama ambacho kimenilea na mimi mwenyewe nakitumikia kwa uadilifu na kwa
juhudi kubwa pengine kuliko ilivyo kwa hao wazushi.Habari Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)