Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Mozambiq, Mama Graca
Machel, wakati walipokutana na katika viwanja vya Mozambiq Heroes
Square, kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha mwasisi
wa nchi hiyo, Samora Machel, zilizofanyika leo, mjini Maputo. Kulia kwa
Makamu ni Mama Zakhia Bilal na (katikati) ni Rais wa Afrika ya Kusini,
Jacob Zuma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal,mkewe Mama Zakhia Bilal na Mama Maria Nyerere,wakiwa pamoja na
baadhi ya Marais wan chi za Afrika wakati walipohudhulia katika sherehe
za maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mwasisi na Rais wa
Mozambiq, Samora Machel.
Askari
wakimuongoza Rais wa Mozambiq, Armando Guebuza, kuelekea kuweka Shada
la maua katika Kaburi la Mwasisi wan chi hiyo, ambaye pia aliwahi kuwa
Rais wa nchini hiyo, Samora Machel.
Kingunge
Ngombale Mwilu, akijumuika na wananchi wa nchini Mozambiq, kuelekea
kuweka mashada ya maua katika kaburi la Mwasisi wa nchini hiyo.
Rais wa zamani wa Zambia, Keneth Kaunda, akiweka Shada la maua.
Mama
Maria Nyerere akiweka Shada la Maua ndani chumba maalum mahala lilipo
kaburi la mwasisi wan chi ya Mozambiq, wakati wa maadhimisho ya sherehe
za kumbukumbu ya kifo cha mwasisi huyo zilizofanyika mjini Maputo
Msumbiji leo.
Makamu
wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jmabo na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma.
Picha Na Muhidin Sufiani












No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)