MIAKA 50 YA UHURU:WANANCHI WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YA AFYA KATIKA MAONYESHO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MIAKA 50 YA UHURU:WANANCHI WAFAIDIKA NA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YA AFYA KATIKA MAONYESHO

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiingia katika eneo kunakotolewa huduma mbali mbali za upimaji wa afya na  matibabu katika mabanda ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru katika utoaji huduma za afya Tanzania.
Afisa Muuguzi Sista Zania Ndimbo kutoka Hospitali ya Amana akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliojitokeza kupima ugonjwa wa Kisukari.
Muuguzi Asma Msimbe akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima Ugonjwa wa Kisukari kwa mmoja watu waliojitokeza kupima Afya zao
 Baadhi ya wananchi wakisubiri katika foleni ya kupata huduma ya Bure ya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Matiti kwa kina Mama.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika foleni katika banda linalotoa huduma ya Upimaji na Mtibabu ya Macho bure.
Moja wapo ya bango lililopo katika eneo la kuingilia katika mabanda yanayotoa huduma hizo likionyesha huduma zinazotolewa bure kwa watu wote kwa kipindi chote cha maadhimisho hayo.
Afisa Muuguzi Sista Zania Ndimbo kutoka Hospitali ya Amana akitoa huduma kwa mmoja wa watu waliojitokeza kupima ugonjwa wa Kisukari.
 
Katika Banda la Ushauri Nasaha na Upimaji VVU lililopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Muuguzi Mshauri Rehema Kessy akitoa maelekezo sahihi ya jinsi ya kutumia mipira ya kiume Kondom kwa kijana  Frank Christopher.
 Bendi ya Mjomba ikitoa burudani katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo wananchi wanapata Ujumbe kupitia muziki huo na burudani pia huku Upimaji wa Afya zao bure ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages