Mabasi Haya Yasadikiwa Yalibeba Mamluki Kuelekea igunga - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mabasi Haya Yasadikiwa Yalibeba Mamluki Kuelekea igunga

 MABASI madogo manne aina ya Rosa ya kampuni ya Mukeshi Travels yaliyokuwa na watu wanaodaiwa ni mamluki wa CHADEMA waliotoka Tarime na Musoma mkoani Mara kwenda kuvuruga uchaguzi Igunga, yakiwa yameegeshwa eneo la Tinde mkoani Shinyanga kwa ajili ya upekuzi wa Polisi jana. Hata hivyo walidai walikuwa wanakwenda kwenye kampeni huku wengine wakidai wanakwenda kuwa mawakala wa chama hicho siku ya uchaguzi.Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Msimamizi wa Uchaguzi mawakala waliapishwa jana. Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba watu hao waliodaiwa kuwa mamluki ni kwamba si mamluki wameapishwa leo jioni kuwa mawakala wa chama hicho.
Na Mpigapicha Wetu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages