Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye
ni mtoto wa Juma Mwapachu, aliyefariki dunia leo asubuhi.Kulia ni Balozi
Juma Mwapachu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na mke wa Balozi Juma Mwapachu, Rose Mwapachu, wakati
alipofika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo jioni kumpa
pole kufuatia kifo cha mtoto wake, Harith Mwapachu kilichotokea leo
asubuhi, Oktoba 11.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe, wakati
walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith
Mwapachu nyumbani kwa Mwapachu Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya waombolezaji, wakati akiondoka nyumbani kwa
Balozi Juma Mwapachu, wakati alipofika kutoa pole kufuatia kifo cha
mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu leo.









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)