Hii ndio Nembo Inayotumika tokea kuanzishwa Kwa LUKAZA BLOG na itaendelea hadi pale Tutakapoitambulisha Upya Nembo yetu Mpya Itakayotumika na LUKAZA BLOG
Hii Ndio Nembo Mpya ya LUKAZA BLOG itakayoanza kutumika Muda si mrefu
Leo ni Siku Ya Kuzaliwa LUKAZA BLOG ambapo ilianzishwa
tarehe kama ya leo mnamo mwaka 2010 ambapo ilikua ni kipindi cha kampeni za
uchaguzi mkuu nchini Tanzania.
Lukaza Blog inapenda kuchukua nafasi hii kwanza Kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunipa Nguvu,juhudi na akili katika kufanya lukaza blog
iweze kufika na kuoneka vizuri kama inavyoonekana hivi leo.
Vilevile napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Familia yangu
pamoja na ndugu zangu wote ambao wameweza kunisaidia kwa ushauri , na kunipa
moyo na kuwezesha blogu hii kufika hapa ilipo leo
Napenda kuchukua nafasi kumshukuru Kaka yangu Haki Ngowi Kwa
Msaada wake mkubwa katika kuifikisha Lukaza blog hapa ilipoo leo vilevile
napenda kuwashukuru wadau wote na kaka zangu ambao wamenitangulia katika tasnia
hii ya blogu kama vile Issa Michuzi wa Mmiliki Wa Michuzi Blog, Muhidin Sufiani
Wa Sufiani Mafoto Blog, Ndugu yangu Fred Tony Njeje wa Mbeya Yetu Blogu kwa
msaada wao kwa njia moja au nyingine kwa Kuiwezesha Lukaza blog kufika hapa
ilipo leo.
Nawashukuru Vodacom Tanzania Kwa kuweza kudhamini Lukaza
Blog wakati ikiwa na miezi Mitano tu Napenda kuwashukuru kwa kuchukua uamuzi sahihi wa kudhamini blogu hii kwa maana ni
blogu ambayo inakua kwa kasi sana nchini Tanzania na Duniani Kote. Vilevile Lukaza Blogu inapenda Kuwakaribishha Wote ambao wanapenda kudhamini au kutangaza biashara zao kupitia Blogu hii na Kwa Bei Nafuu kabisa.
Ni vigumu kuwashukuru wote ila napenda Kuwashukuru Wanafunzi
Wote Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Kwa Msaada wao Mkubwa katika Kuipeperusha Lukaza
BLogu Sehemu zote walipo na kuweza kuisaidia lukaza blogu kufikia hapa ilipo.
Vilevile Napenda Kuwashukuru Wadau wote ambao wameza
kushirikiana Na Lukaza Blogu na kuwaomba kuendeleza ushirikiano Wetu katika
kuwatumikia wananchi wa Dunia Hii katika Kuwafikishia Habari .
Lukaza Blogu Inapenda Kuitambulisha logo yake Mpya ikiwa ni
Kuadhimisha Mwaka Mmoja tokea kuzaliwa kwake lakini logo hii inaanza kuwa
hewani muda wowote kuanzia leo.
Mungu akitujalia Baadae Lukaza Blog itakuja Na Mambo mengi
matamu tu Ambayo naamini Wadau Wote wa Lukaza Blogu mtafurahia Huduma
zitakazotolewa na Lukaza Blogu.
Napenda Kuwashukuru Tena Wadau na Ndugu Zangu wote
Walioifikisha Lukaza Blogu hapa ilipofika Leo na Kuwaomba Waendelee na Moyo
Huohuo Katika Kutimiza wajibu wetu na kwa kila mtu na nafasi yake.
Ahsante sana Na Sina jinsi ya Kuwalipa maana fadhila zenu ni
Nyingi lakini Mungu Atawalipia na kuwazidishia Mara mbili ya Kile Mlichokitoa
katika Kufanikisha Lukaza Blog kupata mafanikio haya madogo.
Mungu Awabariki, Awajalie na Awazidishie.
JOSEPHAT LUKAZA
LUKAZA BLOG ADMINISTRATOR
- SUPER BRAND BLOG -







Keep on working brother for sure I love your work and I will always follow upon your way to reach my future destiny. When we come across I need to talk and gain experience from you. Be leased and keep on moving forward as always I will be there for you.
ReplyDelete