Wafanyakazi
wa Benki ya KCB Tanzania wakipanga viroba vya vyakula wakati hafla ya
kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya
shilingi milioni 4.5/- kwa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika
Mazingira magumu cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es
Salaam.
Wafanyakazi
wa Benki ya KCB Tanzania wakiandaa viroba vya vyakula wakati hafla ya
kukabidhi msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali kwa watoto yatima hao.
Watoto
wanaoishi katika kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira
magumu cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam
wakifurahi baada ya kukabidhiwa msaada wa Vyakula na vifaa mbalimbali
vyenye thamani ya milioni 4.5/- kutoka kwa Benki ya KCB Tanzania hivi
karibuni.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Moezz Mir, akiwakabidhi moja ya
Mifuko ya Chandarua watoto wa kituo cha Friends of Don Bosco kIlichopo
Kimara jijini Dar es Salaam wakati benki hiyo ilipokabidhi msaada wa
vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/- hafla
iliyofanyika kituoni hapo hivi karibuni.
JAMII
ya Kitanzania, imeaswa kuwaangalia kwa jicho la huruma watu wasiojiweza
na wenye mahitaji maalum ili kuwaweza kuishi vizuri na kujiona kuwa ni
sehemu ya jamii pamoja na mapungufu waliyokuwa nayo.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa kituo cha kulelea
watoto ya tima na wanoishi katika mazingira magumu cha Friends of Don
Bosco iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa
bodi ya Benki ya KCB Dk Edmund Mndolwa alisema makundi maalumu
yanahitaji upendo na msaada wa wana jamii ili waweze kuishi vizuri.
Dk
Mndolwa alisema kuwa, Benki ya KCB inatambua umuhimu wa kuyasaidia
makundi hayo na ndiyo maana kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii ime
kuwa ikiyapatia misaada mbalimbali ya kijamii.
“Leo
Benki ya KCB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali na vyakula vyenye
thamani ya shilingi milioni nne na nusu. Msaada huu siyo mkubwa sana
lakini ni wazi kuwa utawasaidia watoto wanaolelewa katika kituo hiki.
Makampuni mengine na watu binafsi wanapaswa kutambua kuwa hata kidogo
walichonacho wakikitoa kinaweza kuleta tofauti,” alisema
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa msaada utitolewa na Benki ya KCB ni muendelezo
misaada mbalimbali ambayo Benki hiyo inaitoa mwaka hadi mwaka na
kuongeza kuwa kwa kipindi hiki cha Octoba hadi Desemba benki ya KCB
imetenga shilingi milioni 180 kwa ajili ya kuisaidia jamii.
Kwa
upande wake, kaimu mkurugenzi wa kituo hicho Theobald Triphone alisema
kuwa msaada uliotolewa na benki ya KCB umekuja wakati muafaka kutokana
na kuwa kituo kinakabiliwa na matatizo mengi.
“Msaada
huu kwetu ni mkubwa sana . Kituo kinakabiliwa na matatizo mengi na
kibaya zaidi hatuna mfadhili wa kudumu jambo ambalo ni tatizo kubwa.
Watoto
hawa ambao baadhi ni yatima na wengine waliokuwa wakiishi katika
mazingira magumu wahitaji chakula,malazi, mavazi na elimu, tunawaomba
wana jamii waiige benki ya KCB kwa kuwasaidia,” alisema
Baadhi
ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda, magodoro, vyandarua,
mashuka, madaftari, kalamu, unga, maharage, mchele sukari pamoja na
mafuta ya kupikia.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)