MAPACHA WA3 NA MSONDO KUWAPA SHAVU T-MOTO MODERN TAARAB KATIKA UZINDUZI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAPACHA WA3 NA MSONDO KUWAPA SHAVU T-MOTO MODERN TAARAB KATIKA UZINDUZI

BENDI inayoendelea kufanya vizuri katika jukwaa la muziki wa dansi nchini Mapacha Watatu na Bendi Kongwe nchini, Msondo Ngoma zimeandaa shoo maalum kwa ajili ya kuwasindikiza ndugu zao kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taab (T-Moto) ‘Real Madrid’ katika uzinduzi wa kundi hilo utakaofanyika Oktoba 28 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Akizungumza na Sufianimafoto, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na mazungumzo na bendi hizo zitakazowasindikiza katika onyesho hilo la uzinduzi ambazo zote zimeitikia wito.
Aidha Amini, alisema kuwa  uzinduzi wa kundi hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa albam yao kwanza ya inayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea.
kundi hilo tayari limekwisha kamilisha albam mbili kwa mpigo, ambapo itakayozinduliwa siku hiyo ya oktoba 28, tayari nyimbo zake zimeshaanza kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages