Jamboree ya hewani ya Kimataifa ya Skauti itafanyika mkoani Arusha tarehe 15 na 16 Oktoba 2011.
Jamboree
ya Hewani ni kambi ambayo skauti duniani pote huwasiliana na skauti
wengine kwa kutumia vifaa vya mawasiliano [Radio calls] pamoja na
mtandao wa Kompyta. [internet]
Hii ni mara ya kwanza kwa Kambi hii kufanyika kitaifa nje
ya mkoa wa D’salaam, Skauti kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatakiwa
kuhudhuria kambi hii muhimu ambayo pia ni sehemu ya mafunzo kwao. Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ni shughuli ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa Oktoba, na madhumuni yake ni kuwaweka karibu skauti duniani kote kwa kutumia Mawasiliano ya Radio na mtandao wa Kompyuta, [internet]
Shughuli hii ambayo hufanyika kwa muda siku 2 [saa 48] huwapa fursa skauti kubadilishana ujuzi
mbalimbali ikiwa ni pamoja mafunzo ya kiskauti, nyimbo, na michezo
mbalimbali. Kupitia kambi hii ya Kimataifa, skauti pia hujifunza lugha
mbalimbali za kimataifa. Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa kambi hiyo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, na inakadiliwa jumla ya skauti 1000 watahudhuria.Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blogu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)