Hapa Mtoto Cecilia akitoka
Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel
Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.
Mtoto Cecilia alitangazwa hivi
karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa
pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya
moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.
Taarifa za Cecilia ziliweza
kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua
kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema
walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa
matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya
operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja
kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na
Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
Kwa hiyo imekuwa ni vigumu
kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa
sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba
watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya
kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa
watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa uchunguzi tunaweza
tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)