
Taarifa ya Mabadiliko ya Mtandao wa Matukio na wanavyuo
Sasa Blog hii imeungana na wanavyuo watanzania wanaosoma nje ya Tanzania
Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.
Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo(www.tzwanavyuo.blogspot.com)
sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo
watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania, Tumefanya hivi
kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya tanzania
kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko,
Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari
zake ama habari zao hapa. Pia kwa watumishi wa vyuo Hapa nchini Tanzania
mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama
kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja
kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo. Mabadiliko mengine tuliyo yafanya
kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo
tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania,pia tumeweka na mambo
mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.Mtandao wa wanafunzi
ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani
mnakaribishwa kujiunga www.tzuniversitiesconnects.tk mnakaribishwa sana pia mtakutana na wanavyuo wengine.Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati.
Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa: twanavyuo@live.com
Tembelea Mtandao wa Matukio na wanavyuo hapa: www.tzwanavyuo.blogspot.com
Kwa niaba ya wanavyuo wote,
Matukio na wanavyuo Crew.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)