Wananchi waliofika kuomboleza msibani katika mtaa wa Mwaka kati mji
mdogo wa Tunduma lakini Baba wa Marehemu Bwana Asanwisye Mwampamba
aliamua kuwatimua kwa madai mwanae Bi Rhoida Mwampamba hajafa.
Muumini
wa kanila la Last Church lililopo mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi
mkoani Mbeya leo amewazuia wakazi wa mtaa wa Mwaka kati Mwaka kulia
katika msiba wa motto wake na kuzuia taratibu zote za mazishi kwa kile
alichodai mwanawe hajafa amelala.
Bwana
Asanwisye Mwampamba mwenye umri wa miaka 72 alipata taarifa za kufariki
mwanawe Rhoida Mwampamba mwenye umri wa miaka 35, mama mwenye watoto
wawili wa kike na wa kiume kutoka kwa binti yake aitwaye Sarah Mwampamba
mwenye umri wa miaka 18 kwamba dada yake amefariki majira ya saa 8
kamili usiku wa kuamkia jana.
Lakini tangu muda huo alianza maombi kuwa mwanawe amelala hivyo hakuna sababu ya watu kulia na kutanga msiba.
Kwa
upande wake mtendaji wa kitongoji cha Mwaka kati Bwana Godnes Mwaipula
alipoitwa katika tukio hilo alifika lakini mzee huyo aliendelea na
maombi akiamini kuwa mwanae amelala, ndipo mtendaji huo alipochukua
jukumu la kwenda kumwita Mwenyekiti wa mji mdogo wa Tunduma Bwana Elias
Cheyo.
Hata
hivyo mwenyekiti Bwana Cheyo alifika katika eneo la maombi ambapo
alishiriki kumwombea Bi Rhoida na ndipo kadri masaa yanavyozidi kuyoyoma
hadi kufikia saa 12 kamili asubuhi, akachoka na hivyo akamshauri mzee
huyo kuamini kuwa mwanae amefariki ambapo mzee huyo aliendelea na
msimamo wakuwa mwanae amelala.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Bwana Cheyo amesema kuwa majira ya saa 7 mchana
serikali iliamua kuingilia kati na kuuzika mwili wa marehemu huyo.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)