---
Na Ezekiel Kamanga-Mbeya yetu.
Jinamizi la ajali mbaya limeendelea kuusakama mkoa wa Mbeya ambapo
usiku wa kuamkia jana imetokea eneo la Mlima Nyoka Uyole Jijini humo
na kuua watu watatu akiwemo dereva wa gari hilo dogo Yuda Ambokile
Jeshi la Polisi limethibitisha.
Kaimu kamanda wa polisi Anacletus Malindisa anesema Marehemu
wengine ni Peter Kishimba mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Tazara
Iyunga na Joshua Sanga mwenye umri wa miaka 2 mkazi wa Uyole jijini
Mbeya na ajali hiyo ilitokea majira ya saa Moja na nusu kwa kuhusisha
gari Nne ambazo zote zilijeruhi watu waliokuwemo ndani yake.
Wakizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, mashuhuda wa
ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuharibika kwa gari
aina ya Toyota Dyana yenye namba za usajili T 660 AUX ambayo ilikuwa
imeegeshwa katika mlima huo.
Walisema kuwa kutokana na kuharibika kwa gari hiyo ndipo gari dogo
aina ya Suzuki Escudo yenye namba za usajili T 425 BAZ , iliyokuwa
ikitokea barabara ya Mbarali kwenda Mbeya mjini ambayo ilikuwa na
abiria watano iliigonga gari hiyo na kusababisha kifo cha Dereva wake
Yuda Ambokile na wengine kujeruhiwa vibaya na magari mengine Toyota
Cheser T 512 BCT na Nissan T 991 BAK.
Baada ya gari hiyo kugonga gari iliyokuwa imeegeshwa na
kusababisha madhara hayo ndipo gari nyingine aina ya Baloon ikagongwa
na gari hiyo aina ya Escudo kisha Baloon hiyo ikatumbukia korongoni na
kusababisha majeruhi wawili waliokuwemo ndani ya gari hiyo ambao wote
walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Mmoja wao
akaruhusiwa baada ya hali yake Kiafya kuimarika.
Ajali hiyo haikuishia hapo bali gari nyingine aina ya Pickup yenye
namba za usajili T 991 BAK nayo ikakumbwa na dhahama hiyo ambapo
iliharibika vibaya bila kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwemo ndani
yake.
Majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya na kutembelewa na waandishi wa habari leo, wengi wao walikutwa
wakiwa na hali mbaya na kushindwa kuzungumza chochote bali baadhi yao
waliokuwa na nafuu walisema kuwa walikuwa hawakumbuki chochote juu ya
ajali hiyo zaidi ya kujikuta wamelazwa wakiwa na majeraha katika miili
yao.
Majeruhi hao ambao baadhi yao waliweza kuzungumza na waandishi wa
habari ni pamoja na Denis Untwa (24) ambaye ni dereva wa Baloon, Laina
John Sanga (35), Michael Mteve (20), Anania Simbeye(35) ambaye ni
dereva wa Escudo, Emmanuel Tambikeni na mmoja aliyejitaja kwa shida
jina moja la Boniface..





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)