Ziara ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Pemba - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Ziara ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Pemba


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na akizungumza na wananchi wa Daya Mtambwe,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofili na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba,mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa banda la karafuu Daya Mtambwe
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwamamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni.
Waziri wa Ardhi,Makaazi,maji na Nishati Mhe Ali Juma Shamuhuna,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaun Takao,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni,akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofili na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu0-Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages