Mapacha Kuingia Mzigoni Rasmi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mapacha Kuingia Mzigoni Rasmi

Na Andrew Chale
VICHWA vipya kwenye maswala ya usanifu  ‘graphics’ na uhariri ‘editing’ kwenye  fillamu na muziki wa bongo Francis na Frank George Ntevi  ambao ni mapacha wametamba kufanya kweli kwenye anga hizo ilikuleta mabadiliko ya kweli kwenye soko la filamu na muziki wa Bongo

Wakizungu na Tanzania Daima  jana jijini Dar es Salaam, Mapacha hao walisema kua mpaka sasa wamesha  fanya kazi za kuongoza na kuihariri  filamu ya ‘The Magic Flower’ ya msanii na kiongozi wa shirikisho la wasanii  Tanzania (TAFF)Simon Mwakifamba.
“Mpaka sasa tumesha fanikiwa kuongoza filamu ya The Magic flower ni hakika itakapoingia sokoni watanzania watakubali kiwango cha filamu na utundu uliotumika kwenye filamu hiyo” walisema Mapacha hao.

Mbali na filamu hiyo pia waliweza kufanyia  graphis filamu za ‘Time after time’ iliyoigizwa na mastaa wa Bongo Izzo Bzness, Quick  Raca, Jackline  Wolper  na  filamu nyingine  ni ya  ‘My Angel’  part 1-2 ya Yusuph Mlela huku filamu zingine wanazozifanyia  graphics na editing zipo mbioni kutoka hapo baadae..

Frank na Francis ama  ‘The Squares’  wamekua wakifanya shuguli hizo za chini  ya studio ya Ntevi Pro vision ya Magomeni jijini Dar es Salaam iliyo chini ya baba yao.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages