Ndugu
Watanzania,
Shukrani za pekee ziwaendee wale wote aliojitolea kwa hali na
mali kumchangia mtoto Sesilia Edward ambaye anahitaji msaada wa haraka
wa operesheni ya moyo.
Tunapenda kuwataarifu kuwa
fedha za operesheni zimekwishapatikana, na tayari tiketi mbili (ya
kwake na mlezi wake Peter Nyambaliko) zimekwisha patikana.
Kwa sasa, motto Sesilia amelazwa katika hopsitali ya Regency
chini ya uangalizi mkubwa wa Daktari Bingwa Dr. Kanabar na timu yake
tayari kupunguza maji yalioyojaa tumboni kabla ya yeye kusafiri siku ya
Jumatano.
Dola 6,100 tayari zimekwishalipwa kwa ajili ya matibabu India,
na tiketi mbili zimekwishalipiwa. Tayari tumelipa shilingi 200,000 kama
admission fee katika hospitali ya Regency ambapo tunatemegemea mtoto
Sesilia atalazwa hadi Jumanne tarehe 20, kabla ya kusafiri Jumatano.
Gharama zilizobaki za Regency zitagaramiwa na hospitali ya Regency.
Yote hii ni katika kuiweka hali yake sawia kabla ya safari ndefu
kuelekea India.
Bado tunahitaji msaada wa fedha za kununua madawa ambapo kwa
wiki mtoto Sesilia hutumia madawa zaidi ya shilingi 50,000. Tunahitaji
nguo kubwa kubwa za kuvaa kwani tumbo linaongezeka sentimeta moja kila
baada ya masaa 72.
Unaweza kumtemebelea mtoto Sesilia katika hospitali ya Regency
kwa leo jumatatu na kesho jumanne
Kama una msaada wa haraka kama nguo, chakula peleka katika kituo
cha Chanel Ten – Dar es Salaam.
Na weka pesa katika account
zuatazo:
Tigo Pesa:- 0715 095797
MPESA: – 0762
962467
NMB Account: 2072517079
Kwa maelezo zaidi, piga simu 0767-262625
Watanzania tumeweza, tunamuombea mtoto Sesilia aende salama na
arudi salama.
Shukrani za dhati kwenu wote kwa niaba ya
Africa Media Group Limited
Hoyce Temu
Mtangazaji
- Mimi na Tanzania
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)