Mtendaji
wa Mtaa wa Kiungani Kata ya Kurasini Manispaa ya Temeke, Theophilda
Christopher, akitoa maoni yake wakati wa mafunzo ya siku moja ya
kuwajengea uwezo watendaji wa Mitaa na Kata juu ya kutoa msaada wa
kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana, yanaendeshwa na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini na
Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara (TLS).
Wakili
kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS) Steven Madulu, akitoa
somo kwa watendaji wa Mitaa na Kata jana mjini Dar es salaam juu ya
utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na
hawawezi kumudu gharama kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za
Temeke na Kinondoni.
Wakili
kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS) John Seka akiwafundisha
watendaji wa Mitaa na Kata jana mjini Dar es salaam juu ya utoaji wa
msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na hawawezi
kumudu gharama kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za Temeke
na Kinondoni.
Baadhi
ya Watendaji Mtaa na Kata kutoka wilaya za Kinondoni na Temeke mkoani
Dar es salaam wakisikiliza kwa makini jana mjini Dar es salaam mafunzo
ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi kwenye maeneo yao. Mafunzo hayo
yanaendesha na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini Chama cha
Wanasheria wa Tanzania Bara(TLS).
******************************
Na Tiganya Vincent – MAELEZO-Dar es salaam
CHAMA cha
Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kimeendesha mafunzo maalum ya siku moja
ya kuwawezesha Watendaji wa Mitaa, Kata wa Wilaya za Temeke na
Kinondoni jinsi ya kutoa msaada wa kisheria kwa jamii inayowazunguma
katika mitaa.
Kauli
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaa na Mratibu wa Mradi wa
Maboresho wa Sekta ya Sheria kutoka TLS, Maria Matui, wakati akizungumza
na waandishi wa habari baada ya mafunzo hayo.
Alisema
kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watendaji hao kufikisha
ujumbe wa msaada wa kisheria kwa wananchi ili waweze kutambua wapi
wanaweza kupata huduma hiyo bila malipo.
Aidha
Matui aliongeza kuwa mafunzo hayo yanawashirikisha watendaji 90 kutoka
maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kinondoni na Temeke ili kuwajengea uwezo
wa kuwaelimisha wananchi jinsi ya kupata msaada wa kisheria ili nao
pia waweze kutoa msaada huo kwa wananchi pindi mwananchi anapohitaji.
Alisema
kuwa chini ya mafunzo hayo wananchi watapata ufahamu juu ya vigezo
vinavyostahili mtu kupata msaada wa kisheria bila malipo kutoa TLS na
pia kujua siku ya msaada wa kisheria kitaifa .
Matui
alisema kuwa mwananchi wamekuwa hawapati huduma za msaada wa kisheria
kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za mawakili na wakati mwingine
baadhi ya maeneo hakuna mawakili hali inayowafanya kukosa haki zao za
msingi.
Alisema
mafunzo hayo yanakusudia kuhakikisha kuwa msaada wa kisheria unafika
katika ngazi ya chini ya jamii kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria
kuweza kutambilika .
Chama
cha Wanasheria Tanzania Bara(TLS) kinaendesha mafunzo hayo chini
Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) wa Wizara ya Katiba na
Sheria.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)