Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania leo imetangaza kuandaa na kuyadhamini mashindano ya baiskeli
ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge 2011, ambayo yamekuwa na mvuto wa hali
ya juu katika mikoa ya kanda ya ziwa. Mashindano haya yataanzia mjini Shinyanga na kumalizikia Jijini Mwanza mwezi ujao na yatagharimu zaidi ya shilingi milioni 50.
Baadhi
ya waendesha baiskeli wa Mkoa wa Shinyanga wakifanya mazoezi tayari kwa
kujiandaa kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli "Vodacom Mwanza
Cycle challenge 2011"zitakazoanzia Shinyanga hadi Jijini Mwanza mnamo
tarehe 22 mwezi wa kumi mwaka huu.
Akizungumza
naWaandishi wa Habari, leo katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga
Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa alisema
kuwa mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha
baiskeli kujitokeza kwa wingi.
“Mashindano
haya yameboreshwa kwa upande wa zawadi, ubora na viwango, na tofauti na
miaka ya nyuma, mashindano ya mwaka huu yatahusisha mikoa miwili muhimu
kwa mchezo wa baiskeli kanda ya Ziwa, yani Shinyanga na Mwanza”Alisema.
Alisema
mashindano hayo yatafanyika tarehe 22 mwezi ujao na kwamba yatakuwa
mbio za kilomita 196 kwa wanaume, 80 kwa wanawake, upande wa walemavu ni
Kilometa 15 kwa walemavu wanaume na Kilomita 10 kwa walemavu wanawake.
“Washindi katika kila kundi watapewa zawadi mbalimbali ambazo tutazitangaza baadae,”Alisema.
Alifafanua
kuwa mashindano ya mwaka huu ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge
yameandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa takribani
miaka mitano na pia Vodacom ina nia ya kuendelea kuandaa na kukuza
mchezo huu ili Tanzania iweze kujulikana zaidi kimataifa katika mchezo
huu wa baiskeli.
“Shindano
hili la Vodacom Mwanza Cycle Challenge ni mahususi kwa kukuza mchezo
huu hapa nchini kwa lengo la kupata wawakilishi bora katika mashindano
mbalimbali ya kimataifa,”alifafanua.
Katika
kuzingatia kuwa mwaka huu Tanganyika inasherehekea miaka 50 ya uhuru,
Vodacom Tanzania itatoa zawadi ya mshiriki mwenye umri wa kuanzia miaka
50 atakaemaliza wa kwanza katika kundi la washiriki 50 wa kwanza. Hivyo
amewataka Watanzania wenye uwezo kujiandikisha kwa wingi ili kuweza
kushiriki na hatimae kujishindia zawadi kem kem
Nae
Mwenyekiti wa Baiskeli Kanda ya Ziwa bwana Elisha Eliya, amesema mwaka
huu ili kuleta mabadiliko na kuboresha zaidi mashindano haya, mbio
zitaanzia Mkoa wa Shinyanga na kumalizikia Mwanza kwa sababu hii ni
mikoa miwili inayoongoza katika uendeshaji wa baiskeli katika kanda hii.
Amewataka wanamichezo wote nchini wanaoshiriki katika mashindano haya kuanza kujiandaa wao pamoja na vifaa vyao vya michezo ili waweze kuwa katika hali nzuri ya kiushindani zaidi.
Ametoa
wito kwa washiriki kutoka mikoa yote nchini kujiandikisha kwa wingi na
kufika Shinyanga mapema ili kuhudhuria semina ya washiriki wote siku
moja kabla ya mashindano.
Bwana Eliya amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani wa hali ya juu kwani njia itakuwa ya moja kwa moja na watahakikisha hakuna mtu atakaeingia kwenye mashindano kati kati ya njia hivyo kupata washindi halali,Na alichukua frusa hiyo kwa kutoa wito kwa makambuni mbalimbali hapa nchini kujitokeza kudhamini mbio hizo.
Vodacom
Tanzania imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali kama vile Soka, Riadha,
kuogelea, mashindano ya boti, mashindano ya Mbuzi, Vodacom Miss
Tanzania, Tenisi na mingine mingi ili kuhakikisha kwamba taifa linafanya
vizuri katika tasnia nzima ya michezo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)