Katibu mtendaji wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari kuhusu zoezi la upigaji wa kura
linaloendelea duniani kote kwa ajili ya kupata Nembo rasmi ya Haki za
binadamu itakayotumika duniani, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi
zilizoridhia mkataba wa wa kimataifa wa Haki za Binadamu
inashiriki zoezi hilo kwa wananchi kupiga kura kuchagua nembo inayofaa
kati ya kumi zilizopendekezwa kupitia mtandao wa www.humanrightslogo.net
kabla ya tarehe 17 mwezi huu.
Katibu mtendaji wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay (katikati) akiwa na
balozi wa Canada nchini Tanzania Robert Orr (kushoto) na
Mshauri msaidizi anayeshughulikia zoezi la uhamasishaji wa kupiga kura
kutoka ubalozi wa Ujerumani Bw. Hans Koeppel (kulia) kwa pamoja
wakionyesha nembo kumi ambazo zinapigiwa kura na mataifa mbalimbali
kupitia mtandao wa www.humanrightslogo.net ambapo nembo itakayopata
kura nyingi itawasilishwa tarehe 23 mwezi huu kwenye mkutano wa Umoja.
Katibu mtendaji wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay (katikati) akijadili
jambo na balozi wa Canada nchini Tanzania Bw. Robert Orr
(kushoto) na Mshauri msaidizi anayeshughulikia zoezi la
uhamasishaji wa kupiga kura kutoka ubalozi wa Ujerumani Bw. Hans
Koeppel (kulia) leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa
uhamasishaji wa watanzania kushiriki zoezi la kupiga kura ya Nembo ya
Haki za binadamu.
Balozi wa Canada nchini
Tanzania Robert Orr akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe
mbalimbali waliohudhuria mkutano wa uhamasishaji wa Tanzania
(watanzania) kushiriki zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kupata nembo
rasmi itakayotumika kimataifa kwa ajili ya shughuli za Haki za Binadamu
leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine balozi huyo amesema
watanzania wanaomchango mkubwa katika kupiga kura ili ipatikane nembo
moja kati ya kumi zilizopendekezwa na washindi wa tuzo za Amani na
wanaharakati mashuhuri wa Haki za Binadamu duniani.Picha na Aron Msigwa –
MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)