Wapenzi
wa kinywaji mahiri cha Guinness na mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu
nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza leo wamekusanyika katika viwanja vya
Leaders kwa ajili ya kushiriki katika GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
ambayo imezinduliwa leo katika viwanja hivyo.
Washiriki
wengi wamejitokeza ili kujisajiri na kuonyesha maajabu ya mpira wa
miguu katika kipindi hiki kabambe cha Televisheni ambacho kinaangaliwa
na kuwavutia watu wengi barani Afrika,Shindano hili litawapatia
mashabiki nchini Tanzania nafasi ya kujitokeza na kuonyesha mapenzi yao
ya dhati katika mpira wa miguu na kushindana na mashabiki wakubwa wa
mpira wa miguu kutoka Kenya na Uganda huku kujishindia mamilioni ya
fedha.
Katika
picha juu kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Guinness Moris Njowoka
akumuelekeza jambo Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti
Breweriers Ephraim Mafuru wakati wa shindano hilo leo.
Baada
ya kupatika na timu nane zitakazokuwa na watu wawiliwawili , timu hizo
zikishiriki katika shindano hilo kupitia Luninga (Television) likirushwa
mara moja kila wiki Televisheni kwa muda wa wiki nane, na kila wiki
atapatikana mshindi mmoja atakayejishindia Dolla za Kimarekani 50.000,
Shafii
Dauda Mtangazaji wa Clouds FM akiwaelekeza jambo washiriki wa shindano
la Guinness Football Challenger katika viwanja vya Leaders leo.
Mmoja
wa washiriki katika shindano hilo akionyesha uwezo wake katika kumiliki
mpira wa miguu kama anavyoonekana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)