Picha hii ni
kielelezo cha jinsi ya uchangiaji damu.
Na mwandishi
wetu.
Uchangiaji wa damu salama mashuleni mkoani Mbeya umepungua
kutokana wanafunzi wanaochanguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kuwa
na umri mdogo na hivyo walio wengi kukosa kutimiza vigezo vya uchangiaji
damu ambapo kigezo mojawapo ni kuanzia umri wa miaka 18.
Akiongea na mwandishi wetu Meneja
wa kitengo cha damu salama nyanda za juu kusini Daktari Lelo Bilihima
amesema kuwa licha ya kampeni na juhudi zinazofanywa na kitengo hicho
kuwa uhitaji wa damu unatakiwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na kiasi
kilichopo katika hospitali nyingi.
Aidha ameongeza kuwa damu hiyo haiuzwi na kwa yeyote atakayebainika anauza damu hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Aidha ameongeza kuwa damu hiyo haiuzwi na kwa yeyote atakayebainika anauza damu hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Wakati huo huo akizungumzia
upande wa wananchi Dkt. Baliyima Lelo amesema kuwa wachangiaji wengine
wanaogopa ukubwa wa sindano hivyo kupunguza uchaangiaji wa damu na
amewataka wananchi kuondokana na uvumi ulioenea kwa sasa kuwa mchangiaji
akichangia mara moja atatakiwa kuchangia tena kwa zaidi ya mara na
kusisitiza kuwa jukumu la kuchangia damu ni wajibu wa kila mmoja.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)